akiongea kwenye blog hii mmiliki wa kampuni hiyo ambaye ni mwandishi wa script za filamu mkubwa hapa nchini Ally Mtakuja amesema anatoa ofa ya kuwashutia wasanii wachanga tu ambao wana nia ya kuweza kujiendeleza kwenye fani hii ya uigizaji..Hapa Ally anaongea kwa ufafanuzi zaidi..unajua kuna makundi mengi sana ya sanaa ya uigizaji hapa nchini ambayo yanajituma lakini mwisho wake wanaishia kufanya mazoezi tu na hatimae makundi hayo yanakufa.hakuna utaratibu mzuri kutoka kwenye chama cha waigizaji wala serikali wa kuweza kuwasaidia wasanii wachanga wa nchi hii kwa kutambua hilo kampuni yangu ya mtakuja production inatoa ofa kwa kikundi au vikundi vyovyote vile vyenye nia ya kujiendeleza, kuwashutia filamu na kuwafanyia editing bure...ndiyo najua watu wanaweza wakashangaa kusikia hivyo lakini nataka kuwaambia wasanii wachanga wa vikundi wachangamkie ofa hii ya kushutiwa filamu bure ikiwa pamoja na kuwafanyia editing na kuwakabidhi master ili wao wenyewe wachague ni wapi wataamua kupeleka kuuza filamu hiyo.
Napenda tu ieleweke kuwa ofa hii ni kwa ajili ya wasanii wachanga tu.Na wala haitoendelea itakapofika mwezi wa februali mwakani.alisema Ally mkurugenzi wa kampuni ya mtakuja production.
tunataka kila mtu awe na uhiano sawa kwenye nchi hii wapo wasanii wachanga wenye uwezo mkubwa zaidi ya hata hao tunaowaona kila siku lakini hakuna anayeweza kuwapa saport ili watimize ndoto zao aliongeza Ally.
Watu wasije wakafikiria kuwa huu ni utani hapana tupo sirious na jambo hili sasa kazi ni kwao tu hao wasanii .Wanachotakiwa kufanya ni kuwasiliana na kampuni yetu kwa njia ya simu ambazo ni 0656 15 51 50 ili tuwape maelekezo ya kufanya kabla hatujafika na kuwashutia filamu zao.
Alipoulizwa vp kuhusu vikundi ambavyo vipo mkoani Ally alisema >> tena vikundi vya mikoani ndiyo tutakavyowapa kipaumbele zaidi kwa sababu tunajua kuwa huko walipo production ni chache sana na hata kama zipo ni production zisizo kuwa na utalaam wa kutosha kwa hiyo hata hao wa mikoani pia wasisite kuwasiliana na sisi tutawasaidia ila ni lazima wafanye haraka kwasababu kampuni ina mambo mengi mno ya kufanya ikiwa pamoja na kuandaa filamu za maproducer mbalimbali
je umeisoma habari hii na je wewe ni mmoja kati ya watu ambao ungependa uupate msaada huu basi usisite kuwasiliana na namba ya hapo juu tafadhari usibeep.
zifuatazo hapo chini ni picha za vifaa vinavyomilikiwa na mtakuja production
![]() KAMERA YA KISASA KABISA AINA YA CANOON 7D |
![]() |
COMPUTER YA EDITNG YA KISASA AINA YA MACINITOSH YENYE PROGRAM KUBWA ZA EDITING |
![]() |
KAMERA YA KISASA YENYE LENZI KUBWA INAYOTAKIWA KWENYE FILAMU |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni