Alhamisi, 12 Desemba 2013

DOTNATA NI ZAIDI YA WASANII WA TANZANIA

DOTNATA AKIWA KWENYE POZI
Mwandishi wa script na mtunzi wa filamu mbali mbali za hapa bongo Ally Mtakuja.Amemzungumzia msanii wa siku nyingi kwenye tasnia ya filamu Husna Posh au kama anavyojulikana na wengi kwa jina la DOTNATA kuwa ni zaidi ya wasanii wengine hapa bongo.akizungumza kwa uwazi na upana bila ya kificho chochote Ally alisema...nimeshafanya kazi nyingi na Dotnata ni msanii wa ajabu sana siku zote anajari kukusaidia kwanza harafu mambo mengine huwa yanakuja baadae..nimekuwa nikiitumia nyumba yake mara kwa mara katika kutengeneza filamu zangu,ukweli ni kwamba huwa ananisapoti sana kila ninachotaka kufanya,ananisaidia hata pale ninapoelekea kukwama,siku zote amekuwa ni mama wa ukweli kwangu,ananishauri mengi yanayofaa na mara kwa mara amenitaka niwe makini na watu ninaofanya nao kazi..alisema Ally..hata hivyo aliongeza kwa kusema kuwa DOTNATA ndiye pekee aliyepigania haki yangu mpaka leo ninapoandika story au script za filamu naandikwa jina langu,,unajua mwanzo nimewaandikia sana wasanii lakini walikuwa hawaniandiki hata kwenye shukrani mpaka nilipokutana na mama DOTNATA ndipo na mimi sasa watu walipoanza kunitambua...amekuwa ni mtu anayeniamini siku zote kwenye kazi zangu na mimi pia kwa uwezo wake mungu najitahidi kumuonesha juhudi zangu na maarifa niliyonayo..Akizungumza kuhusu watu wanaosaidiwa na DOTNATA kisha hawampi hata shukrani Ally alisema....Unajua mimi nawashangaa sana binadamu wengine utakuta mtu anamfuata mtu kwa heshima na adabu ili asaidiwe matatizo yake na kweli anaposaidiwa akafanikisha mambo yake anamsahau aliyefanikisha mpaka yeye kufikia hapo alipo.Mimi nawajua ni watu wengi sana wamesaidiwa na DOTNATA lakini sijawahi kuwasikia wakimshukuru kwa wema wake alioufanya wamekuwa majeuri na kujiona kuwa wameshafanikiwa.Nadhani wanasahau kuwa shida haina siku moja ipo siku unaweza ukapata shida nyengine na hakuna wa kuweza kukusaidia mbona mimi nimekuwa wazi kusema kuwa ni DOTNATA ndiye aliyenisaidia mpaka kuwa hapa bila yeye nafikiri nisingefikia hapa au nisingejulikana na watu wengine wanaonipa kazi.amenipa kipaumbele sana na mpaka kesho na kesho kutwa bado nitaendelea kuhitaji msaada kwake kwani hata hapa nilipo bado nahitaji mengi mno kutoka kwake.Ukiachilia na umri mkubwa alionao yeye ni kama mama yangu,lakini pia ameanza sanaa muda mrefu kuliko hata sisi tulioingia juzi juzi kwa hiyo mtu kama huyu ni muhimu ila watu wanashindwa tu kumuelewa.Alikazia Ally
DOTNATA KWENYE POZI

.

hata hivyo Ally alimalizia kwa kusema kuwa.Serikali inabidi isapoti sana kwa watu kama hawa iwe inawapa kipaumbele kwenye mambo mbalimbali..kuna vingi vya kufanya lakini serikali ingefikilia suala la kutoa tuzo za heshima za wana jamii wanaosaidia wana jamii wenzao nafikiri wangempa mama DOTNATA tuzo ya heshima ya Mwanamke mjasiriamali na anayesaidia watu..

UWEZO MKUBWA WA KUPAMBA NA KUSIMAMIA MAHARUSI NI MOJA YA KAZI ZAKE
Mwisho kabisa Ally Mtakuja alimaliza kusema kuwa watu wakumbuke fadhira kwani anayekusaidia ukimshukuru tu kwake imetosha tusiwe wachoyo wa fadhira.


POSTED  BY ; ALLY MTAKUJA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni