Jumanne, 17 Desemba 2013

HIVI UNAJUA ALICHOKISEMA RICH MAVOKO

MSANII wa Bongo fleva, Richard Martin ‘Rich Mavoko’ amewataka wasanii wenzake wawe na moyo wa kuwakumbuka wenzao waliotangulia mbele za haki hata kwa kuwatembelea wazazi au ndugu zao waliopo duniani.

Hivi karibuni, Rich Mavoko alimtembelea mama wa aliyekuwa msanii wa vichekesho, marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ aliyefariki Novemba mwaka jana na kuonyesha simanzi nzito kutokana na alichosimuliwa na mama huyo.

Kwa mujibu wa Rich Mavoko, kupitia ukurasa wake wa kijamii, aliandika kuwa wasanii wanatakiwa wapendane kutokana na kazi zao kuwaunganisha na watu mbalimbali, pia wanatakiwa kuwa na umoja ili kufanikisha ndoto zao.

“Muda mwingine wasanii tunahitaji tukumbuke wenzetu waliotangulia, tena kwa kuwaenzi hata kwa kuwatembelea ndugu zao, kwa sababu kuna vitu vinauma sana ukielezwa, mama Sharo anasema baada ya kufa mwanaye, haki zake nyingi hajui zipo wapi, zinaenda vipi na mambo mengi yanayomhusu marehemu, kiukweli iliniuma sana, pole sana mama binadamu ndio tulivyo,” aliandika.

Rich Mavoko ni kati ya wasanii ambao wanaiwakilisha vizuri tasnia ya muziki wa Bongo fleva, kutokana na kuwa na nyimbo zenye mvuto na zinazovutia katika soko la muziki huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni