Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa iliyokuwa inaongozwa na kocha mbrazil Marcio Maximo bwana Meshack Abel ameingia rasmi kwenye mziki na sasa tayari ameshaiachia single yake mpya inayokwenda kwa jina la part ambayo amemshirikisha mwanamuziki mkongwe na wa siku nyingi Daz Bab...Akiongea na blog hii ndugu yake wa karibu na Meshack anayejulikana kwa jina la Haruna Adam amesema kuwa Meshack ni mtu mwenye vipaji vingi sana na sasa ameamua kuionesha jamii kuwa siyo soka tu bali hata kwenye mziki pia yumo.Haruna aliendelea kusema kuwa Watu wanamfahamu mMeshack toka alipokuwa beki kisiki kwenye timu ya Mtibwa na pia aliwahi kuichezea Simba sports club au wekundu wa msimbazi na sasa yupo kenya anacheza kwenye timu ya Bandari ya huko kwa haraka haraka utagundua kuwa Meshack amejikita sana kwenye soka.Lakini nataka niwaambie watu kuwa na hata kwenye mziki Meshack yupo vizuri na mipango yake siyo tu kuachia single moja bali anataka kuja kutoka na album kabisa kama mipango itakwenda kama ilivyopangwa.
![]()
 |
MESHACK ABEL KWENYE POZI |
Naye rafiki wa karibu wa Meshack Abel,bwana Malezu Mtakuja au maarufu Adebayor amesema yeye ndiyo mtu wa mwanzo kabisa kuusikia wimbo huo wa Meshack ameusifia kuwa ni mzuri na pia Adebayor akaongeza kusema kuwa sasa umefika wakati wa kuleta mapinduzi ya mziki.
 |
MESHACK ABEL AKIWA KWENYE POZI |
Unajua wimbo wa Meshack ni mzuri sana hata mimi nilipousikiliza kwa mara ya kwanza sikuamini kama kweli Meshack ana uwezo mkubwa kiasi kile mimi namfahamu kwenye soka zaidi lakini kwenye mziki nilikuwa sijawahi kuujua uwezo wake kwa kweli amenishangaza sana.Tunamtakia kila la kheri kwenye soka na mziki pia mungu atamuwezesha na kufanikisha kila anachokifanya alisema Adebayor ambaye ni rafiki wa karibu na Meshack.
 |
BEKI WA KIMATAIFA WA TANZANIA ANAYECHEZEA BANDARI YA KENYA MESHACK ABEL |
Mtakujablogsport ilijitahidi kumtafuta Meshack kwa njia ya simu lakini hatukufanikiwa kumpata kwa sababu tayari alikuwa ameshaondoka nchini na sasa yupo Kenya kwenye club yake ya Bandari anayochezea kwa ajili ya muendelezo wa ligi kuu nchini humo.Hta hivyo tunawaahidi kuwa wiki ijayo tutauweka wimbo wa Meshack kwenye blog hii ili watu wote muweze kuusikia ikiwezekana hata kuudownload pia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni