Alhamisi, 19 Desemba 2013

Picha za mapokezi ya Mchezaji Mpya wa YANGA Emmanuel OKWI..!!


ABDALLAH BIN KLEB MWENYE SHATI LA BLUU HUYU NDIYE KIONGOZI MWENYE MIPANGO HATARI KWENYE USAJILI AKIMTAKA MCHEZAJI NI LAZIMA AMPATE
HATIMAYE mshambuliaji raia wa Uganda Emanuel Okwi ametua nchini leo majira ya saa tisa na nusu alasiri na kupokelewa na viongozi wa Yanga katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.




Okwi akilakiwa kwa shangwe na mashabiki waliofika kumpokea mapema leo jioni.
Okwi akiwa na baadhi ya viongozi wa timu ya Yanga waliofika uwanja wa ndege kumpokea mapema leo jioni,jijini dar
Okwi akionesha namba yake ya mashambulizi siku ya jumamosi

Okwi ambaye amesajiliwa Yanga kwa miaka miwili na nusu kwa jumla ya dola 60,000 alitua nchini na ndege ya shirika la Rwanda mbali na viongozi hao wa Yanga ambao ni Abdallah Binkleb, Musa Katabalo na Seif Ahmed 'Magari' pia alilakiwa na wanachama wachache ambao walijitokeza uwanjani hapo kwa lengo la kushuhudia ujio wake.



Akizungumza mara baada ya kutua uwanjani hapo Okwi ambaye amezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 alisajiliwa Simba akitokea SC Villa ya Uganda mwaka 2010 akiwa kinda wa miaka 17, akisajiliwa kwa dau la dola za Kimarekani 40,000 alisema "Mimi ni mchezaji na mpira ni kazi yangu, nimekuja kuichezea Yanga na nitaitumikia kwa mapenzi yangu yote, nimekuja kufanya kazi na si kuiangalia Simba, mkataba wangu na Simba ulishaishaga.



Akizungumzia mechi ya Yanga na Simba itakayofanyika Jumamosi ijayo alisema "Mimi nipo fiti, nipo tayari kucheza mechi ya Simba, nimejiandaa kikamilifu, ila mwenye maamuzi ya mwisho ya mimi kucheza au kutocheza ni kocha, kama atanipanga nitafurahi zaidi."alisema Okwi ambaye amejiunga kambini na wenzake jana jioni kwenye hotel ya Protea iliyopo Oyesterbay jijjini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya Nani Mtani Jembe Jumamosi.



Kuhusu utata wa usajili wake Yanga, Okwi alisema "Mimi hayo mambo siyajui, nimeyaacha mikononi mwa viongozi wa Yanga ndio watakaomaliza hilo suala."alisema Okwi ambaye baada ya mkataba wake na Simba kuisha Desemba mwaka jana aliongezewa mkataba wa miaka miwili na Simba kabla hajaanza kuutumikia akahamia Etoile du Sahel ya Tunisia ambako aliuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 fedha ambazo Simba wanazisotea mpaka leo kwa kile walichoeleza kuwa Etoile haijawalipa.



Kufuatia hali hiyo, Simba walipeleka malalamiko yao Fifa kuishtaki Etoile ambayo nayo ilipeleka malalamiko ya Okwi kuwa ametoroka kwenye klabu hiyo, ambayo hata hivyo alidai alikalishwa benchi miezi mitatu bila kuchezeshwa wala kulipwa mshahara wake kitu ambacho kilimfanya atimkia nchini kwao Uganda miezi michache iliyopita na Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA), lilimuombea kibali mchezaji huyo Fifa ili ajiunge na klabu ya Sports Clab Villa ili kulinda kiwango chake na Fifa ilimuidhinisha kuichezea klabu hiyo kwa muda wa miezi sita suala lake likiwa linashugulikiwa na tayari ameichezea klabu hiyo kwa miezi miwili.



Tayari Fufa wameiandikia Fifa barua kutaka ufafanuzi wa usajili wa mchezaji huyo Yanga kwa vile alizuiwa kucheza michuano ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kwa vile hajamaliza matatizo yake na Etoile du Sahel.



Naye Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga, Abdallah Binkleb alisema "Baada ya mechi ya Jumamosi tutatoa ufafanuzi zaizi kuhusu usajili wa Okwi, sisi hatujakurupuka, tumemsajili kwa ajili aweze kutusaidia kwenye mechi zetu za kimataifa, tunaenda kupeperusha bendera ya Tanzania hivyo Simba wawe wazalendo, kumsajili Okwi ni kama kunogesha 'ice' kwenye keki, tunalenga kuhakikisha michuano ya klabu bingwa

mwakani tunafika mbali.




Kauli ya Binkleb imekuja kukiwa kwa mahasimu wao Simba kunawaka moto kwa wanachama kumshinikiza mwenyekiti wao Ismail Aden Rage kujiuzulu huku wakimtuhumu kutafuna dola laki tatu za mauzo ya Okwi kitu ambacho Rage anakipinga vikali kwa kusema hajatafuna fedha hizo na kuweka ngumu kujiuzulu.


"Natamani kuolewa na Kingwendu"...Rayuu

 MSANII wa kike wa filamu Bongo Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefunguka kwa kusema kuwa mwanaume sahihi kwake na anayestahili kumuoa ni Rashid Mizengwe ‘Kingwendu’ kwa kusema anaamini ndiye anaweza kuwa mwaminifu na kuishi naye kwa raha tofauti na mwanaume mwingine yoyote endapo atapata bahati ya kuolewa naye.

“Unapofika umri fulani suala la kuolewa si mjadala bali ni lazima iwe hivyo lakini shida inakuja je utaolewa na mwanaume anayekujali, kuheshimu na kukupenda? Basi kwangu nataka kuolewa na mwanaume kama Kingwendu naamini nitakuwa na amani raha mstarehe, tofauti na kama nitapata sharobaro sina hakika kama atanijali,”anasema Rayuu kwa fulaha.
Rayuu alisema hayo alipoongea na Maskani Bongo katika mahojiano yake na gazeti hili kuhusu mume gani bora kwake na angependa kuolewa naye na kuishi kama mke na mume, msanii alisema kuwa anahitaji mtu aliyetulia sambamba na umri wa makamo na mtu anayempenda sana kama awe mumewe ni msanii mwenzake Kingwendu au anayefanana naye.




Hii Ndio Siri ya LULU kuwa na shepu Bomba na ya Kuvutia..!!

SIRI ya muonekano mzuri wa msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ imefichuka baada ya kubainika kuwa, amekuwa akifanya mazoezi kila siku kwa kwenda gym.



Lulu alianika siri hiyo hivi karibuni kupitia mtandao wa instargram kwa kutupia picha zikimuonesha akiwa kwenye tizi na baadae alipozi na kujifotoa picha ambazo zilimuonesha akiwa na umbo la kuvutia zaidi huku zikisindikizwa na maneno yasemayo; ‘ndiyo siri ya urembo’.
Hata hivyo, baadhi ya watu walioziona picha hizo walimpongeza kwa uamuzi wake huo huku ushauri pia ukitolewa kwa kila mmoja kujali afya yake kwa kufanya mazoezi pale muda unapopatikana

 Lulu akifanya mazoezi. 

Binti wa Kidato cha tatu Abakwa na Kupachikwa Mimba huko Jijini Mwanza...!!



MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya Bujingwa, iliyopo Nyakato Mwanza (jina linahifadhiwa), mkazi wa Mabatini jijini Mwanza, alibakwa, kutoroshwa nyumbani kwao na hatimaye kupewa mimba na mtu aliyefahamika kwa jina la Roja (27).
Denti huyo akiwa na mwanaye.


Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Mwanza akiwa hoi kimaisha baada ya kufukuzwa kwa mwanaume huyo, denti huyo ambaye sasa ana mtoto mwenye umri wa miezi saba, alisema baada ya kutoroshwa kwao, mwanaume huyo alimpa mateso mengi, ikiwa ni pamoja na vipigo vya mara kwa mara.
Mtuhumiwa aitwaye Roja.


Akisimulia kwa masikitiko, alidai kuwa Roja alimpa mimba akiwa bado mwanafunzi wa kidato cha tatu mwaka 2012 na kumshawishi atoroke nyumbani kwao ili akaishi naye.
Alidai kuwa, usiku wa Desemba 9 mwaka huu, Roja akiwa na baba, alifika nyumbani na kumtaka aondoke mara moja huku akimtupia virago vyake nje ya nyumba bila kujali kuwa na kitoto kichanga.
Hati ya makubalianao.


“Siku hiyo alifika nyumbani na kunitaka niondoke , nilipokataa akaanza kunipiga na chuma kichwani na kunikaba shingoni bila kujali nilikuwa na mtoto mgongoni. Nilipoona hali inazidi kuwa mbaya nikaamua kuondoka zangu na kuja hapa ili nisaidiwe,” alisema mwanafunzi huyo ambaye wakati huo alikuwa katika ofisi za taasisi inayojishughulisha na utetezi wa haki za binadamu iitwayo Farijika.
Katika kuchimba ukweli wa madai hayo, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ilizungumza na wazazi wa denti huyo ambao kwa muda tofauti walikiri taarifa za mtoto wao kutoroshwa na kubakwa hadi kuzalishwa na mwanaume huyo.
PF3.

Kuhusu manyanyaso anayopata mtoto wao, walisema anastahili matibabu (PF3) ambapo vipimo vilionesha kuwa kweli alifanyiwa vitendo hivyo kwa kuwa alikuwa na majeraha ya ndani kwa ndani.
Baada ya kuthibitisha hilo, Roja aliitwa mbele ya watetea haki hao na kukiri kumnyanyasa mkewe lakini akiahidi kutomnyanyasa tena kabla ya kusaini hati ya makubaliano iliyoshuhudiwa na mashahidi watatu, hati ambayo kama akiivunja atafikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo kubaka na shambulio la mwili.
Mama na mtoto wanaonyanyaswa na kijana Roja.

kijana anayetuhumiwa

"Wasanii wa Kike wanakuwa wasagaji kwasababu wanaumizwa kwenye Mapenzi na Wanaume"......Amanda



MSANII wa filamu, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefungukia sababu za baadhi ya mastaa kujiingiza kwenye tabia chafu ya usagaji akidai kuwa, kutendwa na wanaume ndiyo chanzo cha yote.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Amanda alisema maudhi ambayo baadhi ya mastaa wamekuwa wakiyapata kutoka kwa wapenzi wao waliotokea kuwapenda ndiyo husababisha baadhi yao kuona suluhisho ni kuhamia kwenye usagaji.
“Wasanii wanajiingiza huko sababu wanaumizwa na wanaume, wanadhani usagaji ni raha, wanaona hii ni njia sahii ya kujituliza,” alidai Amanda huku akikwepa kujibu swali la kama naye yumo kwenye kundi la wasagaji ama laa.

"Diamond hanitishi kwa Lolote...atawatisha hao watoto wenzake wa Tandale"....Baby Madaha

MWIGIZAJI na mwanamuziki Bongo, Baby Joseph Madaha amemchana Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kumwambia awatishie watoto wa Tandale kwani hana ubavu wa kuchuana naye.


Akizungumza na paparazi wetu, Baby alifunguka kuwa anamshangaa Diamond kujibu kuhusu jinsi alivyomchana wiki kadhaa zilizopita gazetini na kusema yeye hamuwezi kwani alimtangulia kuchomoka kistaa.
“….akiwa bado ana-struggle kupata mkwanja awatishie watoto wenzake wa Tandale, mimi nishazindua brand yangu ya manukato na mikoba ya zawadi, bidhaa ambazo zinaingia sokoni rasmi Desemba 31, awatishe haohao watoto wenzake, mimi siyo saizi yake,” alisema Baby.



Diamond alipotafutwa, simu yake iliita bila kupokelewa.



Add caption

Msanii RIYAMA Awachana wasanii wa kike wanaopenda kupeana 'madenda' hadharani...!!

 RIYAMA amesema kuwa anachukizwa na vitendo vya kimapenzi vinavyoonyeshwa kwenye filamu nyingi za sasa, ikiwemo mabusu ya staili ya kulana denda.


Riyama alisema kuwa zamani walikuwa wanapigana mabusu mashavuni kama ishara ya mapenzi na kusameheana, lakini sasa wanakula denda kabisa.


“Vitendo hivi ni uchafu wa wazi kwenye jamii, hata kama kuna namna ambavyo wanafanya lakini bado kuna tatizo, mtazamaji ambaye ni mtoto, kijana, mzee haelewi hilo, yeye anajua wanapeana denda kitendo hiki sikipendi,” alisema.


Riyama aliwajia juu wale wote wanaopenda kuigiza uzungu uliopitiliza kwa kuwa imekuwa ikizua lawama miongoni mwa wadau wa filamu.

RIYAMA ALLY

“Hii ni ajira yetu, ni heshima kwa familia zetu, bado tuna nafasi ya kuifanya iwe bora na ya kuheshimika kuliko kuiga vitu ambavyo vinafanya ionekane katika mtizamo usio wa kiungwana wakati waigizaji ni waungwana kama watu wengine lakini matendo ndiyo yanayotuangusha,”alisema.


Imekuwa ni jambo la kawaida kwa filamu zinazoigizwa nchini kuhusisha vitendo vya aina hiyo licha ya baadhi ya watu kulalamika.

Hatimaye Mwenyekiti wa CCM jijini MWANZA aliyeuawa na Wananchi kwa Kupigwa mawe azikwa...!!

waombolezaji wakiingiza sanduku lenye mwili wa marehemu
Jeneza lenye mwili wa Clement Mabina likiwa mbele ya waombolezaji.
ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa (CCM), Clement Mabina (56), amezikwa mchana huu shambani kwake Kanyamati, Kisesa mkoani Mwanza. Mazishi hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, viongozi wa serikali, madhehebu ya dini, vyama vya siasa, wananchi na wakazi wa Kisesa ambao wameungana na ndugu, jamaa na marafiki kumsindikiza marehemu Mabina. Mazishi hayo yalitanguliwa na ibada iliyofanyika uwanja wa Ngomeni-Kisesa, Mwanza.

Jumatano, 18 Desemba 2013

MTAKUJA PRODUCTION YATOA OFA KWA WASANII

Kampuni ya mtakuja production inapenda kuwatangazia watu wote wenye vipaji vya uigizaji kuwa inatoa ofa maalum kwa ajili ya sikuu za x mass na mwaka mpya.

akiongea kwenye blog hii mmiliki wa kampuni hiyo ambaye ni mwandishi wa script za filamu mkubwa hapa nchini Ally Mtakuja amesema anatoa ofa ya kuwashutia wasanii wachanga tu ambao wana nia ya kuweza kujiendeleza kwenye fani hii ya uigizaji..Hapa Ally anaongea kwa ufafanuzi zaidi..unajua kuna makundi mengi sana ya sanaa ya uigizaji hapa nchini ambayo yanajituma lakini mwisho wake wanaishia kufanya mazoezi tu na hatimae makundi hayo yanakufa.hakuna utaratibu mzuri kutoka kwenye chama cha waigizaji wala serikali wa kuweza kuwasaidia wasanii wachanga wa nchi hii kwa kutambua hilo kampuni yangu ya mtakuja production inatoa ofa kwa kikundi au vikundi vyovyote vile vyenye nia ya kujiendeleza, kuwashutia filamu na kuwafanyia editing bure...ndiyo najua watu wanaweza wakashangaa kusikia hivyo lakini nataka kuwaambia wasanii wachanga wa vikundi wachangamkie ofa hii ya kushutiwa filamu bure ikiwa pamoja na kuwafanyia editing na kuwakabidhi master ili wao wenyewe wachague ni wapi wataamua kupeleka kuuza filamu hiyo.

Napenda tu ieleweke kuwa ofa hii ni kwa ajili ya wasanii wachanga tu.Na wala haitoendelea itakapofika mwezi wa februali mwakani.alisema Ally mkurugenzi wa kampuni ya mtakuja production.

tunataka kila mtu awe na uhiano sawa kwenye nchi hii wapo wasanii wachanga wenye uwezo mkubwa zaidi ya hata hao tunaowaona kila siku lakini hakuna anayeweza kuwapa saport ili watimize ndoto zao aliongeza Ally.

Watu wasije wakafikiria kuwa huu ni utani hapana tupo sirious na jambo hili sasa kazi ni kwao tu hao wasanii .Wanachotakiwa kufanya ni kuwasiliana na kampuni yetu kwa njia ya simu ambazo ni 0656 15 51 50 ili tuwape maelekezo ya kufanya kabla hatujafika na kuwashutia filamu zao.

Alipoulizwa vp kuhusu vikundi ambavyo vipo mkoani Ally alisema >> tena vikundi vya mikoani ndiyo tutakavyowapa kipaumbele zaidi kwa sababu tunajua kuwa huko walipo production ni chache sana na hata kama zipo ni  production zisizo kuwa na utalaam wa kutosha  kwa hiyo hata hao wa mikoani pia wasisite kuwasiliana na sisi tutawasaidia ila ni lazima wafanye haraka kwasababu kampuni ina mambo mengi mno ya kufanya ikiwa pamoja na kuandaa filamu za maproducer mbalimbali


je umeisoma habari hii na je wewe ni mmoja kati ya watu ambao ungependa uupate msaada huu basi usisite kuwasiliana na namba ya hapo juu tafadhari usibeep.

zifuatazo hapo chini ni picha za vifaa vinavyomilikiwa na mtakuja production

KAMERA YA KISASA KABISA AINA YA CANOON 7D

COMPUTER YA EDITNG YA KISASA AINA YA MACINITOSH YENYE PROGRAM KUBWA ZA EDITING
KAMERA YA KISASA YENYE LENZI KUBWA INAYOTAKIWA KWENYE FILAMU

UMESHAGUNDUA ANACHOHITAJI MWENZI WAKO?-


KUJUA anachohitaji mwenzako ni kila kitu katika uhusiano na ni vyema basi kila wakati kujifunza mbinu za kuendelea kuwa bora zaidi kwa mwenzi wako. Yes! Hapa katika All About Love ni sehemu sahihi ya kukuza uelewa wako.

Tunapitia mambo muhimu ambayo wanawake wengi huvutiwa nayo kwa wanaume. Kuyajua kutakufanya uendelee kuwa mbabe kwenye sayari hii. Ni mada yenye lengo la kuwasaidia zaidi wanaume ambao hawafahamu ni nini hasa wanawake wanapenda kutoka kwao.

Kwa bahati mbaya, wanaume wengi hawapati muda wa kutosha kufikiria kuhusu mapenzi – wengi wanaishia kujadili kuhusu ngono! Hili ni tatizo. Ngono haiwezi kuwa yenye furaha kama uhusiano unayumba.

Ngoja niwaambie, tendo la kukutana kimwili, siyo kila kitu kwenye uhusiano. Upendo ndiyo kila kitu katika mapenzi rafiki zangu. Si vibaya kuwaza namna ya kumfurahisha mwenzako, lakini iwe ndani ya mambo mengine mengi katika kujenga na kuimarisha penzi lenu.
Hebu sasa tuendelee na mada yetu...

MSIFIE MWENZAKO
Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya namna wanandoa wa jinsia mbili tofauti wanavyotambulishana kwa jamaa zao.

MWANAUME: “Peter kutana na mke wangu, anaitwa mama Diana. Nipo naye mwaka wa tatu sasa, tuna watoto wawili, huyo Diana na mwingine anaitwa Chris. Mama Diana, huyu ni Peter nilisoma naye Tosamaganga Sekondari.”
MWANAMKE:“Suzan, huyu ndiye mume wangu mpenzi...anaitwa Elifaraja lakini mimi napenda zaidi kumuita Elly. Nampenda sana mume wangu jamani, tuna watoto wawili, Diana na Chris... (Akimgeukia mumewe) Baby, huyu hapa ni rafiki yangu Suzan. Yaani tumekua naye mtaa mmoja huko Arusha.”

Bila shaka kwa namna wawili hao walivyotambulishana unaweza kuona tofauti kubwa. Mwanaume amemtambulisha mkewe kawaida kabisa, hajaonesha manjonjo au namna anavyompenda na kumthamini, lakini mwanamke amefanya hivyo.
Sikia nikuambie, kumsifia mwanamke, kuna nafasi kubwa sana kwake. Chunguza kwa makini, hata kunapokuwa na mgongano katika familia, halafu wanakatokea wageni, baada ya utambulisho na mazungumzo ya hapa na pale, wageni wakiondoka kunakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kumaliza mpasuko katika familia.

Jenga utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, unamuweka katika kilele cha upendo. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye.

MALENGO
Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati mwingine ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika.
Hii si sahihi. Dunia ya leo imebadilika rafiki zangu. Inawezekana wazee wa zamani walikuwa sahihi, maana ilikuwa ni suala la kununua ng’ombe na kuwaweka katika zizi kwenye kijiji cha jirani, halafu wanapewa malisho mazuri, baada ya miaka miwili wanazaliana, hapo ndipo anamweleza mkewe.

Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo mengi. Kuna suala la hasara katika biashara, utapeli n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu zaidi kuliko yeyote. Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga maisha pamoja.
Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.

Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba.

KIPAUMBELE
Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumaini kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni’.

Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kikazi au kifamilia, mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaenda vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.

TENDO LA NDOA
Hiki ni kipengele nyeti, kinachohitaji lugha nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi cha ndoa. Maana hata maandiko yanasema: “Mwanamke ataacha wazazi wake na kwenda kwa mumewe, nao watakuwa mwili mmoja.”

Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni muhimu likaheshimiwa na kutengewa muda maalum wa kufurahia. Si papara. Kwa bahati mbaya wanaume huwa si wafuatiliaji sana wa kujua namna ya kuwafurahisha zaidi wenzao. Wenyewe wanajiwazia wenyewe. Wanafikiria namna ya kuwakomoa wenzao.

Si sahihi. Tendo la ndoa halina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Akatafute nini nje wakati wewe ndiye mganga wake unayeweza kumtibu barabara?

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vitatu; True Love, Let’s Talk About Love na All About Love vilivyopo mitaani

Rais Kikwete atuma salamu za rambirambi jijini Mwanza kufuatia kifo cha mwenyekiti wa CCM aliyeuawa na wananchi wenye hasira kali...!!

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo kufuatia vifo vya watu wawili vilivyotokea tarehe 15 Desemba, 2013 katika Kitongoji cha Kanyama Kata ya Kisesa Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza.

Rais ametuma salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa kufuatia vifo vya BW. Clement Mabina na Tenery Malimi vilivyotokea baada vurugu zilizosababishwa na mabishano ya ardhi.

Rais amemuomba Mkuu wa Mkoa kuwatahadharisha wananchi kutokuchukua sheria mikononi mwao na pia kuwa waangalifu na matumizi ya silaha za moto.

“Nimesikitishwa na kufadhaishwa sana na taarifa za vifo vya wananchi hao wawili (2) vilivyosababishwa na mgogoro wa Ardhi ambao ungeweza kupata suluhu kwa njia za amani. Ni vema wananchi kuwa na subira na kuwa waangalifu katika kutatua migogoro yao”. Rais amesema na kuongeza kuwa “ ni vema subira na busara zikawa ndio muongozo wa kutatua migogoro yetu katika jamii badala ya hasira”.

Aidha, Rais Kikwete amemuomba Mkuu wa Mkoa amfikishie salamu zake za dhati kwa familia na ndugu wa Marehemu Mabina pamoja na Wazazi na ndugu wa Marehemu Tenery Malimi, ambao walifariki kutokana na vurugu hizo.

“Amewaomba familia zote mbili ziwe na subira wakati huu mgumu kwa kuondokewa na wapendwa wao na kuviacha vyombo vya dola kuchukua hatua kwa kufuata taratibu zilizopo”. Kwa ndugu Mabina, Chama cha Mapinduzi kimepoteza mmoja wa viongozi wake mahiri na wa kutumainiwa. Aidha, kwa marehemu Tenery taifa limepoteza mmoja wa vijana wake wanaochipukia ambae angejaaliwa kuishi angeweza kutoa mchango muhimu kwa maendeleo ya jamii na nchi yetu.

Mabina amewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Diwani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Magu mwaka 2000 – 2005, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza, mwaka 2007 – 2012.

Rais ameziombea nyoyo za marehemu wote Mungu azilaze mahali pema peponi Amen.

Usiyoyajua kuhusu Chacha Makenge, Kijana wa Kitanzania anayeishi kwenye handaki baada ya Nyumba yake kuchomwa moto na Rafiki yake...!!


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni nje ya handaki hilo lililopo mita chache kutoka majengo ya biashara ya Mlimani City, Makenge alisema alichukua uamuzi huo baada ya rafiki yake (jina linahifadhiwa) kumchomea nyumba na kuteketeza samani zote.


“Ilikuwa mwaka 2009 mwanzoni rafiki yangu huyo ndiye alinipa sehemu ya kiwanja chake nijenge nyumba. Nikawa naishi hapo huku nikiendelea na shughuli zangu za kila siku.

“Siku moja akabadili mawazo, akanitaka nihame katika eneo lake bila kunipa sababu, nilimwomba anipe muda nitafute pa kwenda.

“Julai 2009 akaja na polisi, akanikamata na kunipeleka Kituo cha Polisi cha Stakishari, nilipowauliza kosa langu, hawakunieleza.

“Baada ya siku mbili majirani walikuja kuniona na kuniambia kwamba nyumba yangu imechomwa moto na kila kitu kilichokuwa ndani kimeteketea, aliyefanya hivyo ni rafiki yangu. Nilijisikia vibaya sana.

“Siku iliyofuata majirani walikuja tena kituoni wakaniwekea dhamana. Nilipofika kwangu nilikuta majivu tu, iliniuma sana, nililia lakini sikupata ufumbuzi. Kwa vile nilikuwa sina pa kwenda ilibidi niwe nalala palepale nilipochomewa nyumba nikisaidiwa chakula na majirani.

“Siku iliyofuata, saa nne usiku nilivamiwa na watu wanne, wakiwa na mapanga na marungu, nilipambana nao mpaka wakaondoka. Kesho yake nilikwenda kwa mwenyekiti wetu wa serikali ya mtaa, Jumanne Malima kumweleza yaliyonipata, alisikitika, akaniandikia barua kwenda Polisi Stakishari.

“Nilipofika kituoni sikusikilizwa, badala yake walinikamata tena na kuniweka ndani wakidai kwamba nimefunguliwa kesi ya kumjeruhi mtu kwa panga. Hawakukubali niwekewe dhamana.

“Julai 31, 2009 nilifikishwa Mahakama ya Mwanzo Ukonga na baadaye nilipelekwa Mahabusu ya Gereza la Keko, nikawa napelekwa mahakamani hadi Septemba mwaka huo ambako nilihukumiwa kwenda jela miezi 9.

“Nilitumikia maisha ya jela hadi Desemba 10, 2009 nikatolewa kwa msamaha wa Rais Jakaya Kikwete. Nilikwenda kuishi kwa ndugu zangu huku wakifuatilia sababu ya kufanyiwa vitendo hivyo bila mafanikio.

“Maisha ya kwa ndugu hayakunifurahisha kwani hata wao walikuwa na majukumu mengi, niliamua kuendelea na kazi zangu za sanaa pia utunzaji wa mazingira na bustani kwa watu wakawa wananilipa fedha.

“Ndipo nilipoamua kutafuta sehemu iliyotulia ili niweze kuishi, nikapata hapa, ni jirani na Mlimani City. Nilichimba handaki kubwa kama unavyoliona, kwa chini kuna kitanda ninacholalia.

“Kwa hakika hapa sipati shida, wala kelele. Kwanza ni tulivu sana, nimefikia hatua ya kuishi kama mnyama kutokana na mateso na bugudha nilizopata, wengi hawajui nilipo, nipo katika pori hili kwa miaka minne sasa,”alisema Makenge. tazama picha mbali mbali za kijana huyo akiwa katika maeneo ya andaki lake.





WASTARA awachana wanaomchokonoa na kumpikia Majungi.....Aomba aachwe afanye mambo yake..!!

MWIGIZAJI, Wastara, aliyekuwa mke wa Sajuki (marehemu sasa), amewajia juu wale wote wanaomchafua jina kwa kuwaambia kuwa wasitafute fedha kwa kumzushia kashfa.

Kauli yake imekuja baada ya kuanza kuandikwa kwa mtazamo tofauti akisema yeye ni miongoni mwa waigizaji wasiokuwa na kashfa.
Alisema kuwa hataki kuingia kwenye mizozo na watu, hivyo ni bora wakamwacha aendelee kujipanga upya katika maisha yake.


WASTARA

“Sipendi kushushiwa heshima na wala kuingia kwenye migogoro na watu ambao wengine nimekuwa nao, waniheshimu na wasiniandike vibaya,” alisema Wastara.

Wastara aliongeza kuwa haijalishi ana uhusiano wa kimapenzi na nani, lakini kama binadamu anahitaji kuwa na maisha binafsi.

“Kuna baadhi ya watu hawawezi kukaa na kufanya shughuli nyingine zaidi ya kutafuta fedha kwa nguvu kwa kutumia majina ya watu wengine, naomba waniache nifanye mambo yangu na kuendesha maisha yangu, wakija kikazi tufanye kazi, lakini kama ni majungu na kunichunguza sitaki,” alisisitiza.

Mbunge Amponda Miss Tanzania kuwa hafai kuiwakilisha Nchi yetu kwani hajui kuongea Kiswahili...Ataka Shindano la Miss Tanzania Lifutwe...!!

 Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred hajui Kiswahili? Well, tuliowahi kukaa naye kidogo tunaweza kumtetea kuwa anakijua haswaa, sema hupendelea zaidi kuongea kimombo. Pengine ndio maana mbunge wa viti maalum kutoka Zanzibar, Rukia Ahmed anahisi mrembo huyo haijui lugha yake ya taifa


Akiongea bungeni leo, Bi. Rukia amesema Brigitte Alfred hafai kuiwakilisha Tanzania kwakuwa hawezi kuzungumza Kiswahili. Mbunge huyo alienda mbali zaidi kwa kupendekeza mashindano ya Miss Tanzania yafutwe na badala yake yawekwe mashindano ya Sayansi kwa manufaa ya taifa.
Akijibu kauli hiyo, Brigitte amesema: Meanwhile as our county suffers from 3rd world problems this is what is being discussed bungeni. I would love to meet this this woman! Asante mama,” ameandika mrembo huyo kwenye Instagram. “All of your comments give me hope that there’s still sensibility out here,” aliongeza.
“Mh.Rukia amekosa mada bungeni?*rollingmyeyesoutloud*,” alitweet.
“Anko in the office must be jumping for joy right now-they love to say ‘I told you so’-In Kiswahili ofcourse.”
Hata hivyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara alisema serikali haiwezi kuyafuta mashindano hayo kwakuwa yana umuhimu mkubwa kwa taifa na yamekuwa yakiitangaza nchi na shughuli za utalii.

Brigitte Alfred

Jumanne, 17 Desemba 2013

"Sitaki kutumia Simu tena kwani ni Kero sana....Mwenye Shida na mimi Anitumie Barua ".....LULU


ELIZABETH MICHAEL MAARUFU LULU AKIWA KWENYE PICHA INAYOMUONESHA MWILI WAKE
MWANADADA anayetamba katika filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kero yake kubwa ni utumiaji wa simu za mkononi na anasumbuliwa sana na watu wasiokuwa na mambo ya msingi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Lulu alisema simu zinasumbua sana na anatamani irudi enzi ya kutumiana barua posta.
“Sitaki kabisa kutumia simu ya mkononi kwa sasa, mwenye shida na mimi atanitumia barua, yaani sijui hata nisimame wapi, kwani hata nikibadili namba ya simu inasambaa kwa kasi sana,” alidai Lulu.
LULU KWENYE POZI

Lulu alibainisha kuwa kwa siku anapigiwa simu zisizo na faida kwake na kwamba, idadi kubwa wanaompigia ni mashabiki wake, lakini wanakuwa na maneno yasiyo na msingi.
“Kwa siku napigiwa simu nyingi sana ambazo ni kero kwangu. Nafurahi sana ninapopigiwa simu na shabiki wangu, lakini wapo wanaopiga simu kutaka mambo ya ajabu, nakubali kwamba wengi wao ni mashabiki wangu, lakini simu kwangu ni kero kubwa, ingawa ni msaada mkubwa pia kwangu kwani ni sehemu ya kitendea kazi,” aliongeza Lulu.