Alhamisi, 9 Januari 2014

Mwasisi wa CHADEMA, mzee Edwin Mtei amtaka Zitto Kabwe ajiunge na CCM au CUF kwa kuwa ndani ya Chadema kwa sasa hahitajiki


Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei amemtaka Zitto aunde chama chake au atafute kingine cha kujiunga nacho kwa kuwa kwa sasa hana nafasi.

Pia ameshauri kuwa kama ana ndoto za kuwania urais ni vizuri akatafute vyama vingine kama CCM au CUF kwa kuwa ndani ya Chadema kwa sasa hahitajiki.

Mtei alisema kuwa kama anataka kubakia na uanachama wa Mahakama wao hawana shida... “Lakini huwezi kuwapeleka viongozi wako kortini na bado ukaendelea kubaki kuwa mwanachama wetu.”

Alimtuhumu kwa kuwagonganisha viongozi mbalimbali ndani ya Chadema na hata kuzua mitafaruku ya hapa na pale huku akisema kwamba uamuzi wa Kamati Kuu ndiyo wa mwisho.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni