Alhamisi, 30 Januari 2014

JAPHET KASEBA ANABADIRIKA KAMA KINYONGA

Bingwa wa kickboxing anayetambulika ulimwengu mzima bwana JAPHET KASEBA au kama wengi walivyozoea kumwita CHAMPION ameendelea kuungurumisha kipaji chake kengine cha sanaa ya uigizaji kwa kasi kubwa.Baada ya kushiriki kwa mara nyengine tena kwenye filamu ya DOTNATA inayojulikana kwa jina la JANI CHANGA..Japhet ambaye ameshiriki kwenye filamu hiyo kama mfanyabiashara mkubwa wa madini ameonesha uwezo mkubwa kwenye sehemu hiyo tofauti na vile watu walivyomzoea..Akiongea kwa niaba ya mume wake dada PENDO KASEBA ambaye pia hata yeye ni mshiriki wa filamu hiyo alisema.....watu wamezoea kumuona KASEBA kwenye mapigano tu...ukwelli ni kwamba Kaseba wa sasa hivi ukiachilia mbali fani yake ya kickboxing lakini pia ni msanii mzuri sana kwenye tasnia ya uigizaji na ameonesha kumudu kila sekta anayopangwa...Alipoulizwa ushiriki wake anajisikiaje kwenye sehemu hiyo ya mfanyabiashara wa madini na siyo ule upande aliouzoea yeye wa ngumi.Bwana KASEBA alisema "Unajua mimi ni bingwa wa kickboxing,lakini pia ni msanii wa uigizaji,sasa unapokuwa msanii huwezi kuchagua mfumo mmoja wa uigizaji wako inakupasa uwe unabadilika badilika ili kuwapa burudani wapenzi wako...Kwa hiyo nilivyoambiwa na mama DOTNATA kuwa safari hii natakiwa nicheze kama mfanyabiashara wa madini wala sikukataa nilifurahi na nimecheza kwa moyo wangu wote nafikiri hata madirector wangu watakuwa mashahidi kwa hilo"DOTNATA ENTARTAINMENT inakuja na filamu mpya ambayo mpaka sasa imeshamaliza kushutiwa na sasa ipo studio kwa ajili ya editing..
CHAMPION JAPHET KASEBA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni