Huyu ni kijana anaitwa
Nyamigawa Manoti.Si mkubwa sana bali ni kijana mdogo ila watu wazima waliomzidi
umri walikuwa wanamwita mzee kwa sababu ya vujo zake kwenye pesa.Huyu ni kijana
aliyezaliwa kwenye familia ya wafanyabiashara waliokuwa na fedha nyingi mno
kutokana na kukwepa kulipa kodi.Miaka yoote ya biashara yao walikuwa wanapata
faida haramu kwa sababu walikuwa na uwezo wa kuingiza mizigo mikubwa ya
biashara bila ya wasiwasi wowote. Ndiyo si pale bandarini walikuwa wanajua
wenyewe walichokuwa wanakifanya.Nyamigawa alikuwa ni kijana mwenye kugawa pesa
kwa wingi kwa wanawake ,marafiki na watu mbalimbali ambao walikuwa wanamsifia
na kumnyenyekea..Kila alipoona watu wamekaa wanacheza draft alikuwa anaona
fahari kupita karibu yao na kusifiwa kuwa ni handsome mtanashati au kapendeza
na kweli Nyamigawa alikuwa anafurahi mno kwa sifa zile na hakusita kutoa
burungutu la pesa hata la shilingi laki nane na kuwapa wale woote waliokuwa
wanamsifia ,ndiyo aliwapa usishangae si alikuwa na hela nyingi za biashara yao
ambayo kampuni yao ilikuwa hailipi kodi ana wasi wasi gani ? Baba yake mzazi
Nyamigawa Mzee Manoti Mazuta alikuwa na pesa nyingi kweli kweli, wakati
mwengine alikuwa na pesa nyingi mno ambazo kuna wakati alikuwa anakwenda
kuzigawa misikitini na kanisani,ndiyo aligawa sehemu mbalimbali kwenye
mataasisi na sehemu nyengine. Mzee Manoti alikuwa anatoa pesa nyingi kwa watoto
yatima,kwenye vikundi mbalimbali vya wanawake watoto na vijana,hakuishia hapo
alikuwa anatoa pesa kwenye vyombo vya habari sana ili viwe vinamtangazia
biashara yake..kwa kweli alifanikiwa naweza kusema maisha aliyapatia.Mzee huyo
pamoja na mtoto wake Nyamigawa walipata kujulikana sana kwenye jamii na kila
mtu aliwapenda kwa kweli alikuwa anaombewa dua nyingi na watu wa kila rika.Haaa
huyu ndiyo mzee Manoti na mwanaye Nayamigawa..MIAKA MIWILI BAADAE Tanzania ikawa
inafanya kampeni za uchaguzi mkuu watu wengi walikuwa wanashabikia vyama
walivyovipenda hapa nchi iliingia kwenye heka heka za nguvu vyama vya upinzani
vikaunda umoja wao na kuupa jina UKAWA vikawa vinashindana na chama tawala
ambacho ni CCM Mzee Manoti kwa kuwa ni
mfanyabiashara akaona na yeye atumie fursa ya kujinufaisha kupitia uchaguzi huu
mkubwa wa madiwani wabunge na ma rais akaenda kwenye chama tawala ili akipe
fedha nyingi ziwasaidie kwenye kampeni Bahati nzuri mgombea wa chama hiko John
Pombe Joseph Magufuli akazikataa zile pesa,ndiyo aliamua kuzikataa kwa sababu
alishaona mbali,alishaona na kujua lengo la tajiri huyu alijua kuwa anataka
kuficha dhambi zake kwenye mgongo wa kusaidia chama na ni kweli hasa hiyo ndiyo
ilikuwa nia ya tajiri Manoti ..Baada ya kukataliwa pesa zake akaondoka kwa
hasira na kurudi kwenye biashara zake.sijui baada ya hapo alikwenda kwenye
chama gani hiyo atajijua mwenyewe..tarehe 25 ikafika uchaguzi ukafanyika
..matokeo yakatangazwa hatimae mgombea wa CCM akashinda na kuwa Rais wa Jamhuri
ya muungano wa Tanzania bwana Magufuli..
Baada ya kuapishwa Rais
akaanza kazi mara moja na sera yake ilikuwa ni kuanza na kupambana na mambo
makuu manne la kwanza ni Kuondoa umaskini kwa watu kufanya kazi,pili kupunguza
tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana,tatu,Kuendeleza vita dhidi ya adui
rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma na
nne ni kuendeleza kudumisha amani,ulinzi na usalama ya maisha ya wananchi na
mali zao..Baada ya rais kuanza kazi yake akaanza na fagia fagia la viongozi
wabovu kwa kuwafukuza na kuwasimamisha kazi,Viongozi hao kumbe ndiyo walikuwa
marafiki wakubwa na mfanyabiashara Manoti ambao kumbe bwana manoti alikuwa akiwatumia
kwenye kupitisha na kufanya mambo yake kinyume na utaratibu wa serikali na
ndiyo maana bwana manoti alikuwa akipitisha mizigo anavyotaka..Balaa likazidi
kumuandama bwana manoti pale aliposikia kuwa mabehewa yake yamezuiwa ili
akayalipie kodi..alichanganyikiwa ikabidi afunge safari na kwenda, Manoti
alipofika tu kwenye sehemu ya kulipia kodi akaanza kutoa pesa ili ayalipie
akaambiwa hapana inabidi alipie mizigo yake yoote ya nyuma iliyokuwa inapita
bila kulipiwa..ghafra akajikuta yupo sehemu mbaya kwake..Bwana Manoti akawa
hana ujanja ikabidi alipe kodi zote anazodaiwa na sasa bwana manoti pesa yake
inakwenda kihalali na hapo sasa hawezi kuwa na pesa nyingi kama alivyokuwa
mwanzo.Maisha yakaanza kubadilika bwana Manoti akaanza kuuza vitu kidogo kidogo,biashara
zake zikaanza kwenda kihalali akaacha tabia ya kumwaga pesa hovyo,pesa
zikamuishia akabaki na pesa za halali za yeye na familia yake tu ..wale
wapambe,taasisi,makundi ya kijamii aliyokuwa anawapa zile pesa haramu woote
wakawa hawapewi tena pesa..Jamii yake iliyokuwa imemzunguka ikimtegemea yeye
wakawa hohe hahe wameishiwa omba omba imekuwa na kikomo..bwana Manoti akaanza
kuwaaminisha watu wake kuwa Rais amemchukulia pesa zake,kumbe ni uongo
akuwaeleza ukweli watu wake kuwa pesa zote zile alizokuwa nazo mwanzo zilikuwa
ni za wizi na alikuwa akiibia serikali..
Hadithi hii
inatufundisha kuwa wale matajili waliokuwa wanamwaga mipesa ya vujo kwenye
jamii sasa hakuna tena kitu hiko..badala ya kuwaambia watu ukweli wamekuwa
wakishirikiana na vyama pinzani kuwadanganya watu kuwa Rais ameshikilia pesa
zao na uchumi umeshuka..huu ni uongo tena ni uongo uliopitiliza Rais hajashika
pesa za mtu.Waseme tu ukweli kuwa zile pesa za dili siku hizi hakuna tena.Na
habari nilizozipata nasikia Yule mtoto wa mzee Manoti anyeitwa Nyamigawa
ameshakuwa Chizi ukipita kwenye mataa ya pale fire utamuona.
Maskini Nyamigawa.
Posted by Ally Mtakuja
Mzalendo na mwenye
uchungu na taifa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni