Alhamisi, 22 Septemba 2016

Inasikitisha sana lakini itakufundisha


Huyu ni kijana anaitwa Nyamigawa Manoti.Si mkubwa sana bali ni kijana mdogo ila watu wazima waliomzidi umri walikuwa wanamwita mzee kwa sababu ya vujo zake kwenye pesa.Huyu ni kijana aliyezaliwa kwenye familia ya wafanyabiashara waliokuwa na fedha nyingi mno kutokana na kukwepa kulipa kodi.Miaka yoote ya biashara yao walikuwa wanapata faida haramu kwa sababu walikuwa na uwezo wa kuingiza mizigo mikubwa ya biashara bila ya wasiwasi wowote. Ndiyo si pale bandarini walikuwa wanajua wenyewe walichokuwa wanakifanya.Nyamigawa alikuwa ni kijana mwenye kugawa pesa kwa wingi kwa wanawake ,marafiki na watu mbalimbali ambao walikuwa wanamsifia na kumnyenyekea..Kila alipoona watu wamekaa wanacheza draft alikuwa anaona fahari kupita karibu yao na kusifiwa kuwa ni handsome mtanashati au kapendeza na kweli Nyamigawa alikuwa anafurahi mno kwa sifa zile na hakusita kutoa burungutu la pesa hata la shilingi laki nane na kuwapa wale woote waliokuwa wanamsifia ,ndiyo aliwapa usishangae si alikuwa na hela nyingi za biashara yao ambayo kampuni yao ilikuwa hailipi kodi ana wasi wasi gani ? Baba yake mzazi Nyamigawa Mzee Manoti Mazuta alikuwa na pesa nyingi kweli kweli, wakati mwengine alikuwa na pesa nyingi mno ambazo kuna wakati alikuwa anakwenda kuzigawa misikitini na kanisani,ndiyo aligawa sehemu mbalimbali kwenye mataasisi na sehemu nyengine. Mzee Manoti alikuwa anatoa pesa nyingi kwa watoto yatima,kwenye vikundi mbalimbali vya wanawake watoto na vijana,hakuishia hapo alikuwa anatoa pesa kwenye vyombo vya habari sana ili viwe vinamtangazia biashara yake..kwa kweli alifanikiwa naweza kusema maisha aliyapatia.Mzee huyo pamoja na mtoto wake Nyamigawa walipata kujulikana sana kwenye jamii na kila mtu aliwapenda kwa kweli alikuwa anaombewa dua nyingi na watu wa kila rika.Haaa huyu ndiyo mzee Manoti na mwanaye Nayamigawa..MIAKA MIWILI BAADAE Tanzania ikawa inafanya kampeni za uchaguzi mkuu watu wengi walikuwa wanashabikia vyama walivyovipenda hapa nchi iliingia kwenye heka heka za nguvu vyama vya upinzani vikaunda umoja wao na kuupa jina UKAWA vikawa vinashindana na chama tawala ambacho ni CCM  Mzee Manoti kwa kuwa ni mfanyabiashara akaona na yeye atumie fursa ya kujinufaisha kupitia uchaguzi huu mkubwa wa madiwani wabunge na ma rais akaenda kwenye chama tawala ili akipe fedha nyingi ziwasaidie kwenye kampeni Bahati nzuri mgombea wa chama hiko John Pombe Joseph Magufuli akazikataa zile pesa,ndiyo aliamua kuzikataa kwa sababu alishaona mbali,alishaona na kujua lengo la tajiri huyu alijua kuwa anataka kuficha dhambi zake kwenye mgongo wa kusaidia chama na ni kweli hasa hiyo ndiyo ilikuwa nia ya tajiri Manoti ..Baada ya kukataliwa pesa zake akaondoka kwa hasira na kurudi kwenye biashara zake.sijui baada ya hapo alikwenda kwenye chama gani hiyo atajijua mwenyewe..tarehe 25 ikafika uchaguzi ukafanyika ..matokeo yakatangazwa hatimae mgombea wa CCM akashinda na kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania bwana Magufuli..
Baada ya kuapishwa Rais akaanza kazi mara moja na sera yake ilikuwa ni kuanza na kupambana na mambo makuu manne la kwanza ni Kuondoa umaskini kwa watu kufanya kazi,pili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana,tatu,Kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa  na ubadhirifu wa mali ya umma na nne ni kuendeleza kudumisha amani,ulinzi na usalama ya maisha ya wananchi na mali zao..Baada ya rais kuanza kazi yake akaanza na fagia fagia la viongozi wabovu kwa kuwafukuza na kuwasimamisha kazi,Viongozi hao kumbe ndiyo walikuwa marafiki wakubwa na mfanyabiashara Manoti  ambao kumbe bwana manoti alikuwa akiwatumia kwenye kupitisha na kufanya mambo yake kinyume na utaratibu wa serikali na ndiyo maana bwana manoti alikuwa akipitisha mizigo anavyotaka..Balaa likazidi kumuandama bwana manoti pale aliposikia kuwa mabehewa yake yamezuiwa ili akayalipie kodi..alichanganyikiwa ikabidi afunge safari na kwenda, Manoti alipofika tu kwenye sehemu ya kulipia kodi akaanza kutoa pesa ili ayalipie akaambiwa hapana inabidi alipie mizigo yake yoote ya nyuma iliyokuwa inapita bila kulipiwa..ghafra akajikuta yupo sehemu mbaya kwake..Bwana Manoti akawa hana ujanja ikabidi alipe kodi zote anazodaiwa na sasa bwana manoti pesa yake inakwenda kihalali na hapo sasa hawezi kuwa na pesa nyingi kama alivyokuwa mwanzo.Maisha yakaanza kubadilika bwana Manoti akaanza kuuza vitu kidogo kidogo,biashara zake zikaanza kwenda kihalali akaacha tabia ya kumwaga pesa hovyo,pesa zikamuishia akabaki na pesa za halali za yeye na familia yake tu ..wale wapambe,taasisi,makundi ya kijamii aliyokuwa anawapa zile pesa haramu woote wakawa hawapewi tena pesa..Jamii yake iliyokuwa imemzunguka ikimtegemea yeye wakawa hohe hahe wameishiwa omba omba imekuwa na kikomo..bwana Manoti akaanza kuwaaminisha watu wake kuwa Rais amemchukulia pesa zake,kumbe ni uongo akuwaeleza ukweli watu wake kuwa pesa zote zile alizokuwa nazo mwanzo zilikuwa ni za wizi na alikuwa akiibia serikali..
Hadithi hii inatufundisha kuwa wale matajili waliokuwa wanamwaga mipesa ya vujo kwenye jamii sasa hakuna tena kitu hiko..badala ya kuwaambia watu ukweli wamekuwa wakishirikiana na vyama pinzani kuwadanganya watu kuwa Rais ameshikilia pesa zao na uchumi umeshuka..huu ni uongo tena ni uongo uliopitiliza Rais hajashika pesa za mtu.Waseme tu ukweli kuwa zile pesa za dili siku hizi hakuna tena.Na habari nilizozipata nasikia Yule mtoto wa mzee Manoti anyeitwa Nyamigawa ameshakuwa Chizi ukipita kwenye mataa ya pale fire utamuona.
Maskini Nyamigawa.


Posted by Ally Mtakuja
Mzalendo na mwenye uchungu na taifa  



Jumanne, 20 Septemba 2016

UVCCM YATOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI





      VMM/U.80/8/Vol.I/55                                           20/09/2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa imekutana Jumatatu Tarehe 19/09/2016 katika Ukumbi wa UVCCM Makao Makuu, Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Sadifa Juma Khamis (MCC)(MB). Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili na Nidhamu ya UVCCM Taifa, pamoja na mambo mengine kilipokea na kujadili Uhai wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya ya Vijana Mkoani Arusha.
Kikao kilipokea Taarifa na kutafakari, kujadili na kufanya maamuzi yafuatayo:-
1.  NDUGU LENGAI OLE SABAYA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA ARUSHA
Kwa nyakati tofauti Ndugu Sabaya alisimamia na kuyaongoza makundi ya Vijana wa CCM na wasiokuwa wa CCM ili kumkataa Katibu wa UVCCM aliyehamishiwa Mkoani Arusha Ndugu Said Goha kuchukua nafasi ya Ndugu  Ezekiel Mollel licha ya yeye kupewa heshima na kuelimishwa na Vikao vya Taifa na Viongozi mara kadhaa kupitia Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kuhusu mamlaka za Kikanuni, Kanuni ya UVCCM Kanuni ya Utumishi na Kanuni ya Maadili.
Ndugu Sabaya amesababisha taharuki iliyopelekea Ofisi ya UVCCM Mkoa wa Arusha kufungwa kwa minyororo hadi Jeshi la Polisi kuingilia kati. Vile vile taharuki hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa Vijana wa Mkoa wa Arusha kugawanyika katika makundi na kupelekea hali ya Kiusalama na Maadili kwa Jumuiya na Chama kuwa ya wasiwasi.
Ndugu Sabaya kufikishwa Mahakamani akikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kujifanya Mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa. Huku kosa la pili katika muda usiojulikana akidaiwa kughushi vitambulisho vya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) chenye namba MT 86117 wakati akijua ni kinyume cha Sheria za nchi.
Kamati ya Utekelezaji ilipitia tuhuma mbali mbali za vielelezo vya utapeli na ulaghai unaodaiwa kutendwa na Ndugu Lengai Sabaya katika maeneo tofauti huku akijua ni kinyume na miiko ya Maadili ya Uongozi wa UVCCM na CCM.
Kwa makosa yote hayo Ndugu Lengai Ole Sabaya ameyafanya kwa kukiuka Kanuni ya Uongozi na Maadili ya CCM Fungu la (3) ukurasa wa 16 na 17, na fungu la nne (4) ukurasa wa 29, 30 na 31. Pia makosa hayo ameyatenda kinyume na taratibu za Uongozi na Maadili za UVCCM, Ibara ya 6.3.2 Ibara ya 7.5.1, 7.5.4 na 8.2.5.
Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa imependekeza kwa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) kumvua uongozi Ndugu Lengai Ole Sabaya, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha.
Wakati tukisubiria maamuzi ya Chama Cha Mapinduzi, Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa imemsimamisha Uongozi wa Nafasi yake ndani ya UVCCM kutokana na kesi iliyoko Mahakamani na kumtaka kuanzia leo tarehe 20/09/2016 asijihusishe na shughuli zozote za Uongozi wa UVCCM hadi hatima ya tuhuma zake itakapoamuliwa na Mahakama na Vikao husika vya UVCCM na CCM.
2.  NDUGU EZEKIEL MOLLEL
Ndugu Ezekiel Mollel alipokuwa Katibu wa Vijana Mkoa wa Arusha alipewa barua ya Uhamisho, kama inavyoelekezwa na Kanuni ya Utumishi ya UVCCM kifungu cha 3(13) ukurasa wa 21 na 22 inayozungumzia Uhamisho wa mtumishi, Nukuu
“Mfanyakazi yeyote atakayekataa kutii amri ya Uhamisho bila sababu zinazokubalika atachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni hizi”, kama ilivyo katika kifungu cha 7(4)(b)(x). Katika kifungu hiki yameainishwa makosa mengi lakini aliyoyatenda Ndugu Mollel ni haya yafuatayo:-  Kuachishwa na Kufukuzwa Kazi” Nukuu “Mfanyakazi yeyote wa UVCCM ikithibitika kuwa amefanya mojawapo ya makosa yafuatayo ataachishwa Kazi”

(i)                 Kuwa ni mwenye hatia ya kitendo cha ukosefu wa Adabu mahali pa kazi au wakati wa kazi.

(ii)                Kwa makusudi kukataa kutii amri/maagizo halali ya Wakuu wa Kazi au kukataa kutii amri ya Uhamisho.

(iii)              Kushiriki kwa njia moja au nyingine katika kutenda mambo yaliyo kinyume na Maadili ya Uongozi UVCCM na CCM.
Makosa haya ameyarudia Ndugu Ezekiel Mollel aliwahi kusimamishwa kazi mwaka 2015 akiwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Manyara, jambo ambalo lilipelekea kumnyang’anya Kituo na Kumsimamisha Kazi kwa muda, pamoja na yote hayo bado Ndugu Ezekiel Mollel hakuweza kujirekebisha hata pale aliporudishwa Kazini na kupelekwa Mkoa wa Arusha.

Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa imebariki maamuzi yaliyochukuliwa na Sekretarieti ya Baraza Kuu ya UVCCM Taifa iliyokutana tarehe 14/09/2016. Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa imependekeza kwa Baraza Kuu la UVCCM Taifa kumfukuza Kazi mara moja Ndugu Ezekiel Mollel.

TUHUMA ZA KUIBUA UFISADI
Kuhusu madai ya tuhuma zinazotolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha kuwa kuna ufisadi na baadhi ya Viongozi wa Makao Makuu ya UVCCM Taifa wanahusika.
Ikumbukwe kuwa Umoja wa Vijana wa CCM ulianza kujitathimini na kuhakiki Mali za Jumuiya tokea mwezi Desemba, 2015.

Umoja wa Vijana wa CCM Taifa kwa agizo la Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa mwezi Julai, 2016 ulikamilisha uhakiki wa Mali zote za UVCCM Taifa, Mikoa na Wilaya na kuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.

Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa Mikoa  iliyobainika kuwa taarifa zake hazikuwa na ukweli na kubainisha matakwa ya uhakiki kama walivyoagizwa.

Kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kilichokutana tarehe 18/08/2016 Mjini Dodoma kupokea na kupitia taarifa za uhakiki Mali za UVCCM ngazi ya Taifa, Mkoa na Wilaya kiliagiza Sekretarieti ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kuwaita Viongozi wa Mkoa wa Arusha ili kuendelea kujiridhisha na taarifa walizowasilisha Makao Makuu kwa vile zimebainika kuwa na mapungufu makubwa.

Katika Taarifa hiyo iliyowasilishwa kwa maandishi na kuthibitishwa na Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Arusha hakuna sehemu ambayo kumeainishwa ubadhirifu ama upotevu wa fedha kinyume na madai yaliyoibuliwa siku za karibuni baada ya Viongozi hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu, kutokana na makosa ya Maadili ya Uongozi.

Hata Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Arusha ilipoitwa katika kikao cha Kamati ya Maadili cha tarehe 19/08/2016 kilichofanyika Mjini Dodoma walikana na kudai wao hawajawasilisha malalamiko yoyote kuhusu tuhuma wanazozitoa na kusema wanaendelea na kufanyia kazi na kurekebisha mambo ya msingi kuhusu Uchumi wa Mkoa wao.

Kufuatia hatua hiyo Kamati ya Maadili na Nidhamu na Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa iliagiza Ofisi ya Katibu Mkuu iendelee kufuatilia kwa karibu jambo hilo ili kubaini ukweli baada ya kujiridhisha kuweko na harufu ya ubadhirifu, jambo ambalo limepelekea Viongozi hao kutosema ukweli pamoja na kusisitizwa mara kadhaa kwa maandishi bado taarifa zao hazikujitosheleza.

Ofisi ya Katibu Mkuu ilitoa miongozo ya uhakiki kupitia barua Kumb. Na. VMM/C/C.30/15/77 ya tarehe 6/04/2016 na VMM/C/C.30/15/107 ya tarehe 28/07/2016 na VMM/C/C.30/15/112 ya tarehe 29/07/2016.

Kamati ya Utekelezaji imeagiza Sekretarieti kuendelea na hatua zake za kufuatilia jambo hilo na taarifa iwasilishwe haraka iwezekanavyo.

Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa imeteua wajumbe watatu wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mhe. Mboni Mhita (MB)(MNEC) kufuatilia kwa karibu suala la Arusha na taarifa iwasilishwe katika vikao husika.

Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa imeendelea kusisitiza UVCCM ni Taasisi kubwa hivyo uendeshaji wake wa kazi ni uzingatiaji wa Kanuni, Taratibu na Miongozo hivyo haitamkingia kifua mtu katika jambo ambalo linahatarisha uhai au uhujumu wa rasilimali za Jumuiya.


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI



Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
KAIMU KATIBU MKUU


Alhamisi, 15 Septemba 2016

MHE PINDI CHANA AHUDHURIA MKUTANO WA AU KUHUSU HAKI ZA WAPIGAKURA

Mhe Pindi Chana wa kwanza kulia akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa Umoja wa Afrika kuhusu haki za Wapigakura, unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Siasa na Uhusiano ya Kimataifa (SUKI) Dkt Pindi Chana amehudhuria mkutano wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU) unaofanyika katika ukumbi wa AU mjini Addis Ababa, Ethiopia

Mkutano huo ambao umehusisha viongozi na wawakilishi wa vyama vya siasa, mashirika na taasisi za kidini na kimila pamoja na wadau mbalimbali wa demokrasia na haki za Wananchi umejadili kuhusu namna bora ya kutunza na kutetea haki za wapigakura barani Afrika.

Dr Pindi Chana amekiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano huo muhimu wa siku nne unaotarajia kumalizika tarehe 18 Septemba, 2016.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa SUKI, Dkt Pindi Chana akiwa na Ndg Nana Agyakoma,(Mother of Mampong) Kiongozi wa Kimila kutoka nchini Ghana ambae amehudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika kuhusu haki za wananchi.

Dkt Pindi Chana akiwa kwenye mkutano wa Umoja wa Africa (AU) kuhusu haki za wananchi uliohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Kimila na Kidini, vyama vya siasa na wadau wa demookrasia na haki za wapiga kura.