Jumatatu, 3 Februari 2014

ALLY MTAKUJA KUGOMBEA UDIWANI MWAKA 2015

vijana sasa wameamka baada ya kuona kuwa maeneo yao wanayoishi kukosa maendeleo.Hii ni kauri iliyotolewa na muheshimiwa mbunge jina kapuni baada ya kuisikia kauri ya kijana mpenda maendeleo ALLY MTAKUJA baada ya kutangaza nia yake ya kugombea udiwani kwenye kata ya tabata kwa kile kinachodaiwa kuwa kata hiyo imekosa kabisa maendeleo kwa kipindi cha miaka 10 mpaka sasa.Ilikuwa juzi kwenye kikao kilichohusisha wananchi wa tawi la tabata msimbazi magharibi katika kujadili maendeleo hususani barabara zilizofungwa kwa makusudi na watu wachache..Ally mtakuja alisimama na kuchangia hoja ambapo alitoa lawama zake kwa viongozi wa maeneo hayo kuonekana wamelala usingizi ndiyo maana eneo hilo lipo nyuma kimaendeleo hata hivyo baada ya kuchangia hoja Ally alimaliza kwa kuwaambia wananchi kuwa mwaka 2015 wampe kura za ndiyo kwani ameamua kujitoa kimaso maso kugombea udiwani wa eneo hilo jambo lililosababisha wananchi wote kulipuka kwa shangwe kubwa na kumshangilia huku wakiimba ,,diwani,,diwani,,diwani


hata hivyo mpaka sasa ALLY MTAKUJA amekataa kuweka wazi kuwa atagombea udiwani kwa tiketi ya chama gani .....hapana bado kuweka wazi ni mapema mno muda rasmi bado ila utakapofika kila kitu kitakuwa wazi...tupo kwa ajili ya kuleta maendeleo "alisema Ally
ALLY MTAKUJA AKIWA NA MSANII MAARUFU WA BONGO MOVIE AMANDA POSH KWENYE MOJA YA KAZI ZAKE





Maoni 1 :