Jumatano, 12 Oktoba 2016

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA WODI ZA WAZAZI KATIKA HOSPITALI TATU JIJINI DAR ES SALAAM.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutbia kwenye hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa wodi tatu za wazazi na watoto katika Hospitali za Rufaa za Mkoa wa Dar es salaam leo Octoba 11,2016.
Kampuni ya Amsons Gropu imefadhili ujenzi wa wodi za wazazi katika hospitali ya Wananyamala, Amana-Ilala na Temeke, wodi za kisasa zitakuwa vitanda 150 na ujenzi wake utagharimu bilioni 4.5 mpaka ukamilike.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(katikati) akisoma maandishi yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya wazazi katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es salaam,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na kulia ni Meneja wa Biashara wa kampuni ya Amsons Group Bw. Suleiman K.Amour.
Kampuni ya Amsons Gropu imefadhili ujenzi wa wodi za wazazi katika hospitali ya Wananyamala, Amana-Ilala na Temeke, wodi za kisasa zitakuwa vitanda 150 na ujenzi wake utagharimu bilioni 4.5 mpaka ukamilike.



PICHA ZA UWEKAJI JIWE LA MSINGI UJENZI WA WODI ZA WAZAZI


































Watumishi sasa kuhakikiwa majina

SERIKALI imesema uhakiki wa watumishi wa umma, utakamilika ndani ya mwezi huu, hivyo nafasi zilizoachwa wazi baada ya kuondolewa kwa watumishi hewa, zitaanza kujazwa.
Aidha, imesema kwamba baada ya uhakiki huo ambao utasaidia kuwa na orodha sahihi ya watumishi waliopo katika taasisi za umma kwa lengo la kuboresha hali ya utumishi nchini, itaanza mfumo wa kuhakiki majina mapya.
Akizungumza katika awamu ya pili ya kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa TBC 1 juzi, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro alisema uhakiki wa watumishi hewa, umesaidia kuongeza ufanisi katika taasisi zake.
Dk Ndumbaro alisema baada ya kukamilika kwa uhakiki huo, pia wataanza mfumo mwingine wa kuhakiki majina mapya ambayo yatajitokeza mara mbili na kuyatoa ili kubaki na majina sahihi.
“Kwa mfano, yupo mtu anatumia majina matatu lakini akatokea mmoja akaondoa lile la katikati na kubaki na majina mawili labda Laurean Ndumbaro hivyo mfumo utaona kuwa ni jina jipya kumbe kuna mtu ambaye amejitengenezea jina hilo,” alisema Dk Ndumbaro na kufafanua kuwa ili kuondoa mkanganyiko huo, mfumo utatambua na kuyaondoa majina yasiyohusika.
Pia alisema mfumo wa usajili kupitia Vitambulisho vya Taifa (NIDA), utasaidia kwa kiasi kikubwa, kwani utatoa taarifa sahihi za watumishi halali wa serikali.
Aidha, alisema Serikali ya Awamu ya Tano imetia mkazo katika uadilifu na kwamba kauli ya Rais John Magufuli inatekelezwa ipasavyo na watumishi wa umma.
Alisisitiza kuwa kwa ujumla hali ya utumishi wa umma imeimarika tofauti na ilivyokuwa zamani na kwamba wataendelea kuwachukulia hatua watumishi watakaokiuka maadili.
“Kauli ya Rais ya ‘Hapa Kazi Tu’ inatekelezwa vizuri katika utumishi wa umma. Majukumu yetu ni kuandaa na kusimamia sera, kanuni, taratibu, sheria miundo na miongozo inayohusu rasilimali watu katika watumishi wa umma. Pia jukumu la kusimamia maadili ya utumishi wa umma hasa wale ambao hawaangukii kwenye tume ya maadili ambao sio viongozi wa juu,’’ alifafanua Dk Ndumbaro.
Hata hivyo, alisema ili kutilia mkazo kipaumbele hicho cha uadilifu, serikali imekuwa ikiwafikisha mahakamani na kuwachukulia hatua za kinidhamu, watumishi ambao wanakiuka maadili pamoja na kutoa mafunzo sehemu mbalimbali juu ya maadili ya utumishi wa umma.
Kwa mujibu wa Dk Ndumbaro, katika tathmini waliyoifanya imebaini kuwa yapo maeneo yameonesha kuwa viwango vya maadili viko chini ikiwemo maeneo ya fedha na sekta zinazowagusa wananchi moja kwa moja.
Alisema baada ya tathmini hiyo, wanatilia mkazo kwa wafanyakazi kuzingatia kanuni za uadilifu na kuona umuhimu wa kuzingatia taratibu na miongozo ya utumishi na kwamba kwa wale wanaokiuka huchukuliwa hatua za kinidhamu, kushushwa vyeo pamoja na mshahara.
‘’Zamani watumishi waliokuwa wakifanya vibaya ndio waliokuwa wanapewa motisha lakini kwa waliokuwa wanafanya vizuri walikuwa wakiulizwa wamewezaje kufanya hivyo. Kwa hiyo, sisi tunatambua watumishi wanaofanya kazi vizuri kwamba kunalipa,’’ alisema.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo, Suzan Mlay alikiri kwamba kulikuwa na malalamiko ya utendaji usioridhisha wa utumishi wa umma lakini wanawasisitiza watumishi umuhimu wa kuzingatia maadili kutoa huduma kwa wananchi kwa haraka na kadri ya uwezo wake.
“Kipindi kifupi baada ya miezi mitatu iliyopita tumepata mrejesho kutoka kwa wafanyakazi, wastaafu watumishi na wadau mbalimbali ambao wanakuja maofisini na wanasema hali ya utumishi imebadilika kuliko ilivyokuwa zamani,’’ alisema Mlay.

Viongozi wa serikali kutohudhuria kilele cha mwenge


Rais John Magufuli ameagiza viongozi wote wa Serikali walioalikwa kuhudhuria sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa zitakazofanyika keshokutwa katika Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu kutohudhuria sherehe hizo na wale ambao walishalipwa fedha ya posho na safari kwa ajili hiyo wazirejeshe.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo imeeleza kuwa Rais Magufuli ametoa maagizo hayo ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza rasilimali nyingi katika shughuli za maendeleo ya nchi.
Viongozi waliotajwa kutakiwa kufuta safari zao za kwenda Bariadi ni pamoja na Wakuu wote wa Mikoa, Wakuu wote wa Wilaya, Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mameya na Wenyeviti wote wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya pamoja na watumishi ambao huambatana nao wakiwemo madereva na wasaidizi wao ambao kwa idadi hufikia takribani 1,500.
Balozi Kijazi amesema kwa kuwa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru huambatana na Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Muasisi wa Taifa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia miaka 17 iliyopita, agizo hilo limewataka viongozi wote wa mikoa na wilaya kubaki katika maeneo yao ya kazi na kujiwekea utaratibu wa jinsi ya kuienzi siku hiyo.
Aidha, Rais Magufuli ameagiza wilaya zote ambazo zimefanya vizuri katika shughuli za maendeleo wakati Mwenge ulipokuwa katika maeneo yao, zitambuliwe kwa kutangazwa rasmi katika siku ya kilele cha Mbio za Mwenge na kwamba zawadi zilizoandaliwa zitapelekwa kwa wahusika kwa utaratibu utakaoelekezwa na Mamlaka inayohusika kutoa zawadi hizo.
Hata hivyo Rais Magufuli ameelekeza kuwa kutokana na umuhimu wa Mwenge wa Uhuru kwa Taifa, Viongozi wote wa Serikali ya Mkoa wa Simiyu na Wilaya zake pamoja na wananchi wote wa mkoa huo wajitokeze kwa wingi na kushiriki katika sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru keshokutwa.
Mgeni Rasmi katika sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

Jumanne, 11 Oktoba 2016

MAMA JANETH MAGUFULI AHUDHURIA MSIBA WA SHEMEJIE RAIS MSTAAFU MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE MJINI BAGAMOYO

post-feature-image
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akilakiwa na Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete alipowasili kwenye msiba wa Marehemu Mariam Ramadhani Saburi, shemeji yake Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo  Oktoba 10, 2016

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akilakiwa na Bw. Mohamed Kikwete  alipowasili kwenye msiba wa Marehemu Mariam Ramadhani Saburi, shemeji yake Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo   Oktoba 10, 2016. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiifariji wana familia wa Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemejie  (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Ramadhani Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimfariji akifariji wana familia wa Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemejie  (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Ramadhani Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimfariji Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Ramadhani Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na  Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete (kulia) akimfariji Bi Maguno Binti Athumani ambaye ni mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)  Marehemu Mariam Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
Mawaidha yakitolewa msibani
Bw. Yusuph Kikwete akielekeza waombolezaji sehemu ya kukaa wakati wa msiba huo
 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mnbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete alipowasili kwenye  msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo.
 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mkwewe Bi Maguno Binti Athumani kwenye  msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiongea jambo na  Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)  Marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimpa mkono wa pole Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo 
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine  kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo 
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine  kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo 
 Sehemu ya waombolezaji   kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine wakibeba mwili wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo 
Waombolezaji wakimswalia maiti 
waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa  marehemu Mariam Ramadhani Saburi  kuelekeza makaburini huko Bagamoyo leo

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwafariji watoto wa  shemejie Rais Mstaafu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, Marehemu Mariam Ramadhani Saburi,    aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
Sehemu ya waombolezaji msibani
Waombolezaji wakijiandaa kupata chakula cha mchana kabla ya maziko.
Picha na IKULU
KAWAIDA: Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akilakiwa na Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete alipowasili kwenye msiba wa Marehemu Mariam Ramadhani Saburi, shemeji yake Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akilakiwa na Bw. Mohamed Kikwete alipowasili kwenye msiba wa Marehemu Mariam Ramadhani Saburi, shemeji yake Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiifariji wana familia wa Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemejie (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimfariji akifariji wana familia wa Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemejie (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimfariji Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete (kulia) akimfariji Bi Maguno Binti Athumani ambaye ni mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016 Mawaidha yakitolewa msibani Bw. Yusuph Kikwete akielekeza waombolezaji sehemu ya kukaa wakati wa msiba huo Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mnbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete alipowasili kwenye msiba wa shemeji yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo. Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mkwewe Bi Maguno Binti Athumani kwenye msiba wa shemeji yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiongea jambo na Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete kwenye msiba wa shemeji yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimpa mkono wa pole Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine kwenye msiba wa shemeji yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine kwenye msiba wa shemeji yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Sehemu ya waombolezaji kwenye msiba wa shemeji yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine wakibeba mwili wa shemeji yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Waombolezaji wakimswalia maiti waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Mariam Ramadhani Saburi kuelekeza makaburini huko Bagamoyo leo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwafariji watoto wa shemejie Rais Mstaafu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, Marehemu Mariam Ramadhani Saburi, aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016 Sehemu ya waombolezaji msibani Waombolezaji wakijiandaa kupata chakula cha mchana kabla ya maziko. Picha na IKULU