Alhamisi, 11 Septemba 2014

OMY DIMPOZ ALIVYOWAPAGAWISHA MABINTI WA MAMTONI


HII SASA NI KUFURU!!! P-SQUARE WAWEKA SOFA {SAMANI} ZA DHAHABU NDANI YA NYUMBA YAO MPYA....

‘We Talking Money You Talking Nonsense’ huenda ikawa kauli nzuri kuelezea hiki walichokifanya P-Square kwa sasa.


Hakuna ubishi kuwa, kwa hiki walichokifanya sasa, na kama macho yetu hayatudanganyi kwa hiki yanayokiona, mapacha hawa wamefanya kufuru. Kama hii inayoonekana ni dhahabu kweli, basi P-Square, hela wanayo.

Peter ameshare picha hizi nne ambazo wiki hii zitakuwa gumzo barani Afrika ambapo kwenye picha moja inayomuonesha pacha mwezie Paul akiwa amesimama kwenye sebule mpya inayoaminika kuwa ya nyumba yao mpya, ameandika ‘Goldenworld #blessed.’
Kwenye picha nyingine, wanaoonekana wakiwa pamoja kwenye sebule hiyo iliyotawaliwa na kile kinachoonekana kama dhahabu zilizozunguka sofa za kuvutia na Peter ameandika: #2kings…… Work hard,play harder.’Picha nyingine inamuonesha Peter akiwa peke yake kwenye meza ya chakula, kubwa, iliyojaa vyombo vya thamani vya kuvutia na ameandika: A king in my own world…. #Blessed.”

Hatimaye Serikali yabariki TANESCO kupandisha bei za umeme....Naibu waziri asema "atakayeshindwa kumudu gharama hizo, atumie kibatari..."

Naibu Waziri wa umeme, Mh George Simbachawene, amesema kwamba serikali imekubali TANESCO waongeze gharama za umeme kwa 68% kama walivyokuwa wameomba.


Simbachawene ameitoa kauli hiyo wakati akiongea katika kipindi cha Kumepambazuka kupitia Radio One leo asubuhi.



Amesema kwamba hata kama TANESCO wakiongeza gharama za umeme hadi kufikia Tsh 800 kwa unit bei hiyo ni nafuu kuliko gharama za kununua mafuta ya taa.

Mh Simbachawene ametahadharisha kwamba kama mtu ataona kwamba gharama za umeme ni kubwa, basi akawashe kibatari au akae gizani.

WABUNGE WATANYONGWA HADHARANI

BAADHI ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wamesema wala rushwa pamoja na wahujumu uchumi adhabu yao iwe ni kunyongwa. Wametaka Katiba mpya inayoenda kuandikwa itamke hivyo ili kufanya viongozi wa kisiasa kuogopa kama ilivyo kwenye nchi nyingine.

Sababu ya wajumbe hao kupendekeza jambo hilo ni kwamba uhujumu uchumi na rushwa nchini limekuwa tatizo kubwa kwa viongozi. Kutokana na ukiukwaji huo wa maadili, wamesema umefika wakati wa kuweka bayana suala hilo kwenye sheria mama.

Miongoni mwa waliochangia ni Paul Makonda aliyesema suala hilo likiwekwa bayana, litaokoa fedha nyingi za walipa kodi ambazo kwa sasa baadhi ya viongozi wanazichota na kwenda kuzihifadhi nje ya nchi.

Pia alipinga kuruhusu viongozi wa nchi kufungua akaunti nje ya nchi.

“Kwa nini viongozi hao washindwe kuhifadhi fedha zao ndani ya nchi, wanafanya biashara gani hadi wakafungue benki nje ya nchi? “Tusiruhusu jambo hili na napendekeza kwamba kiongozi atakayebainika amekula rushwa na kuhujumu uchumi huyo anyongwe,” alisema Makonda.

Yusuf Singo pia alisema maadili yanazidi kuporomoka kwa viongozi, jambo linalorudisha nchi nyuma.

Alitaka Katiba isisitize maadili kwa kada hiyo na ambao watakiuka wanyongwe. Alitoa mfano wa Japan kuwa kiongozi wa kisiasa anapochunguzwa kwa kujihusisha na rushwa anatoa machozi kwa sababu hajui hatima yake.

“Tunataka na sisi ifike wakati kiongozi akianza kuchunguzwa atoe machozi,” alisema. Dk Mary Mwanjelwa katika mchango wake alisema rushwa imekuwa adui mkubwa wa maendeleo ya Watanzania.

Alisema isipopingwa kuanzia kwenye Katiba, nchi itakuwa inajichora. Alisema Bunge halitaeleweka kama halitaweka jambo hilo kwenye Katiba, kwa sababu wananchi wengi wameteseka ndani ya nchi yao kwa sababu ya rushwa.

Alisema pia wapo viongozi wengi wasio na maadili na ndiyo maana wanajihusisha na vitendo vya rushwa.

Kwa upande wake, Profesa Mark Mwandosya alisema tatizo la rushwa haliwezi kutenganishwa na haki za binadamu kutokana na kukosesha wananchi maendeleo.

Profesa Mwandosya alisema Katiba lazima itambue adui wa haki za wananchi ni rushwa.

Alipendekeza suala hilo litambulike kikatiba na serikali zote mbili zitunge sheria kali za kupambana na rushwa kuhakikisha wananchi wanapata haki zao za msingi bila kutoa wala kupokea rushwa.

Naye Gerison Lwenge alisema Katiba itambue jambo hilo na ikemee vikali kwa wanaotoa na wale wanaopokea.

Alisema kwa ahli ilivyo, wanaobanwa zaidi ni wale ambao wanapokea na akapendekeza sheria kali zitungwe kubana pia wanaotoa.

Alishauri Kamisheni isimamie suala hilo la rushwa badala ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Kwa mujibu wa Lwenge, Kamisheni ni chombo kikubwa zaidi kuliko ilivyo kwa taasisi. Alisema kazi yake itakuwa ni kuzuia zaidi na si kutibu pekee.

Jesca Msambatavangu alisema Takukuru wanafanya kazi vizuri na walishindwa kupambana na rushwa kwa vile hawana uhuru wa kutosha.

Alisema kama Takukuru wakipewa meno kupitia Katiba mpya, watashughulika kwa uhuru zaidi katika kupambana na tatizo la rushwa nchini.

HIZI DAWA ZA KUONGEZA UCHUNGU KWA WAJAWAZITO ..KUMBE NI HATARI

MATUMIZI ya dawa za kienyeji kwa ajili ya kuongeza uchungu na kujifungua mapema, imeelezwa kuchangia zaidi vifo kwa wajawazito.

Mganga Mkuu wa Mkoa Kigoma, Dk Leonald Subi alisema hayo mjini Kigoma kwenye kikao cha wadau wa afya.

Kikao hicho kilihusisha kufanya tathmini na kuona hatua za kuchukua kukabiliana na vifo vya wajawazito na watoto wakati wa kujifungua mkoani humo.

Kiliitishwa na shirika la Wolrd Lung Foundation. Dk Subi alisema kuwa licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau wengine, kukabiliana na hali hiyo, bado wajawazito wanajifungulia majumbani na kutumia dawa hizo hatarishi kwa maisha yao.

Alisema kumekuwa na upungufu wa vifo vya wajawazito na ongezeko la vifo vya watoto.

Alisema vifo vya wajawazito vimepungua kutoka vifo 74 mwaka 2009 hadi kufikia 49 kwa mwaka jana huku vifo vya watoto wachanga vikiongezeka kutoka 720 mwaka 2009 na kufikia 840 mwaka jana.

Mkurugenzi wa Miradi wa World Lung Foundation, Dk Nguke Mwakatundu alisema shirika lake linaboresha huduma za mama na mtoto mkoani humo, lakini changamoto ya vifo vya wajawazito ni kubwa, kutokana na kujifungulia majumbani.